Загрузка страницы

Chalinze yawahakikishia Wawekezaji mazingira rafiki

Chalinze yawahakikishia Wawekezaji mazingira rafiki

Na Omary Mngindo, Magulumatali - Julai 18

HALMASHAURI ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani, imeahidi  kuendelea kuweka mazingira rafiki kwa uwekezaji wanaofika, ili kuhakikisha mikakati wa Viwanda inazidi kufanikiwa.

Hayo yameelezwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchumi ya Madiwani hao Malota Hussein Kwaga, walipotembelea  Mradi wa Saruji wa Kampuni ya Mamba Sementi inayojenga kiwanda kikubwa katika Vijiji vya Magulumatali na Talawanda Kata ya Talawanda.

"Kila kimepanga maeneo ya uwekezaji, kwa upande wetu tumepanga Wataalamu kila idara wanaohusika na zoezi hilo, ili kuhakikisha taratibu za uwekezaji zinafanikiwa kwa haraka," alisema Kwaga.

Akizungumzia uwekezaji huo wa Mgodi wa Kiwanda cha Mamba, Mwenyeiti huyo alisema kwamba utakuwa mkombozi wa ajira, pia kuongeza pato la Vijiji vya Talawanda, Magulumatali, wilaya, Mkoa mpaka Taifa.

"Hatua waliyofikia baada ya kumaliza changamoto ya  fidia ni kubwa, kazi zinaonekana hivyo sisi Madiwani tunaubariki, tunaomba upewa baraka zote na Wizara ya Madini, ili uendelee na kuleta tija kwa Taifa," alisema Kwaga.

Diwani Kata ya Talawanda Athuman Biga aliipongeza Kampuni ya Mamba Sementi kwa kuwashirikiana na wanaChalinze, katika shughuli za kimaendeleo ikiwemo miundombinu ya Madarasa, Zahanati na vifaa mbalimbali.

"WanaTalawanda tumekuwa wanufaika kupitia Kampuni hiyo kutokea mwaka 2010, wamekuwa nasi bega kwa bega wakishirikiana nasi kwenye shughuli mbalimbali za kimaendeleo, mradi tunausubili kwa hamu kubwa," alisema Biga.

Meneja mratibu wa Mradi huo Aboubakary Mlawa alisema taratibu za uhakiki zinaendelea, huku shughuli za mradi zikiwa zineshaaaza ikiwemo kupasua miamba na kukusanya mawe tayari ya majaribio.

Aliingeza kwamba mradi huo utakuwa na utekelezaji wa awamu za upasuaji miamba, kufanya majaribia katika  viwanda rafiki, sambamba na ujenzi wa Kiwanda katika eneo hilo tayari kwa utengenezaji wa Saruji. 

"Harakati za mradi zilianza muda mrefu, ikiwemo kuwaanda Wataalamu kutoka vijijini humo, lilianza kwa kuwalipia gharama za masomo kwa watoto kutoka katani humo, mpaka kufikia ngazi ya chuo," alisema Mlawa.

MWISHO.

Видео Chalinze yawahakikishia Wawekezaji mazingira rafiki канала MNGINDO ONLINE TV
Показать
Комментарии отсутствуют
Введите заголовок:

Введите адрес ссылки:

Введите адрес видео с YouTube:

Зарегистрируйтесь или войдите с
Информация о видео
17 июля 2022 г. 12:27:24
00:02:51
Яндекс.Метрика