Загрузка...

🔥MHE HEMED AFIKA SKULI YA FIDEL CASTRO PEMBA! ATOA POLE BAADA YA DAKHALIA KUUNGUA MOTO

Kukamilika kwa ujenzi wa Barabara ya Kichaka-Chwaka iliyopo katika Jimbo la Kiwani kutatanua fursa za kiuchumi na kuongezeka kwa thamani ya maeneo yaliyopitiwa na barabara hio



Akikukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi ya Maendeleo inayojengwa katika Mkoa wa Kusini Pemba, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. HEMED SULEIMAN ABDULLA amesema ujenzi wa barabara ya KICHAKA - CHWAKA utaondoa changamoto ya muda mrefu ya kukosekana kwa usafiri wa uhakika katika vijiji hivyo pamoja na kuchelewa kufikiwa na huduma mbalimbali za kiuchumi na kijamii kutokana na ubovu wa barabara hio.



Amesema kukamilika kwa barabara hio kutarahisisha upatikanaji wa huduma ya usafiri na usafirishaji, kuimarika kwa fursa za kiuchumi sambamba na kuongezeka thamani kwa maeneo yaliyopitiwa na barabara hio.



Aidha, Mhe. Hemed amesema Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi imeshakamilisha tathmini ya ulipaji wa fidia kwa wananchi wote waliopisha ujenzi wa barabara hio na ambao nyumba na vipando vyao vimeathiriwa na ujenzi huo.



Mhe. Hemed amewataka wananchi wa Chwaka na Wanakiwani kwa ujumla kuwapa ushirikiano wakandarasi katika maeneo yote yanayopitawa na ujenzi wa miradi ya maendeleo ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa na Jimbo hilo kuweza kupiga hatua zaidi kimanedeleo.



Kwa upande wake Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi na uchukuzi Mhe. Badria Atai Massoud ameipongeza Serikali ya Awamu ya Nane (8) kwa kuendelea kuipa kipaombele sekta ya Ujenzi kwa kuimarisha bajeti ya wizara hio ambayo inawawezesha kuendelea kujenga barabara mijini na vijijini.



Mhe. Badria amesema Barabara ya Kichaka Chwaka ni miongoni mwa barabara za Kimkakati zinazoendelea kujengwa Unguja na Pemba ambapo kwa Jimbo la Kiwani wanatarajia kujenga barabara zenye urefu wa KM 21 na tayari tathmini ya maeneo yatakayojengwa barabara hizo imeshafanyika



Mhandisi kutoka kampuni ya Luptan Consults ndugu Kelvin Mmbaga ambao ndio wasimamizi wa ujenzi huo amesema barabara hio ya KM 2.7 imegharimu Dola za Kimarekani Milioni 7.42 ambayo inatarajiwa kukamilika mwezi Julai mwaka huu.



Wakati huo huo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alikagua ujenzi wa Soko la kisasa la samaki na mboga mboga KENGEJA ambapo amesema soko hilo limejengwa kutokana na wafanyabiashara kukosa mazingira mazuri na salama ya kufanyia biashara zao.



Amewaagiza watendaji wa Tawala za Mikoa kuhakikisha wanawapa kipaombele wafanyabiasha waliokuwepo awali pamoja na kuzingatia bei za ukodishwaji wa vikuta sokoni hapo ili wananchi waweze kumudu malipo hayo na kupata nafasi ya kuendelea kufanya biashara zao.



Amewataka wananchi wa Kengeja na vitongoji vyake kuitunza miundombinu ya soko hilo pamoja na kuimarisha usafi ndani na nje ya soko ili liweze kudumu kwa muda mrefu.



Akizungumzia ujenzi wa Kiwanja cha Mpira wa miguu kinachojengwa UKUTINI Wilaya ya Mkoani , Mhe. Hemed amesema uwepo wa uwanja huo ni fursa kwa vijana na wananchi wa wilaya ya mkoani itakayozalisha vijapaji na kutoa ajira kupitia mpira wamiguu.



Mapema Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifika katika skuli ya Sekondari ya FIDEL CASTRO kutoa mkono wa pole na kuwafariji walimu, wanafunzi na wazazi kufuatia kuungua kwa moto Dakhali ya wasichana skulini hapo.



Amesema Serikali itahakikisha inalijenga upya ama kulifanyia ukarabati mkubwa dakhalia hio ili liweze kurudi katika hadhi yake ya awali na wanafunzi waweze kuendelea na masomo yao katika mazingira salama.



Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ametamatiisha ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo inayojengwa katika Mkoa wa Kusini Pemba kwa kukagua miradi ya maendeleo kumi na tano ( 15 ) ikijumuisha Sekta ya ELIMU, BARABARA, MICHEZO, BIASHARA pamoja na SEKTA ya AFYA.

Видео 🔥MHE HEMED AFIKA SKULI YA FIDEL CASTRO PEMBA! ATOA POLE BAADA YA DAKHALIA KUUNGUA MOTO канала Tifu Tv
Яндекс.Метрика
Все заметки Новая заметка Страницу в заметки
Страницу в закладки Мои закладки
На информационно-развлекательном портале SALDA.WS применяются cookie-файлы. Нажимая кнопку Принять, вы подтверждаете свое согласие на их использование.
О CookiesНапомнить позжеПринять