Загрузка страницы

JINSI YA KUWALISHA VIFARANGA WA KUKU WA KIENYEJI WAKUWE HARAKA

Jinsi ya kuwalisha vifaranga wa Kuku wa kienyeji Wakuwe Haraka

Kuna baadhi ya Watu hawapendi kufuga kuku wa kienyeji kwa kusingizia kuwa wanachelewa kukuwa na vifaranga wa kienyeji wanashambuliwa sana na magonjwa, sasa kwenye kipindi cha leo nitakuelekeza jinsi kuwalisha vifaranga wa kuku wa kienyeji ili waepukane na magonjwa na wakue haraka uwahi kuwauza na upate faida.
Stay tuned

Tatizo kubwa la vifaranga vya kuku wa kienyeji kushambuliwa na magonjwa, kudumaa na kuchelewa Kukuwa ni chakula.
Wafugaji wengi wa kuku wa kienyeji huwapa kuku chakula ambacho sio mlo kamili (Balance Diet)

Mlo kamili (Balance Diet) ni chakula ambacho kinavirutubisho vyote muhimu kwaajili ya Kulinda mwili dhidi ya magonjwa, Kuupa mwili nguvu, kujenga mwili, kuupa mwili joto, kuimarisha mifupa na kusafisha na kurahisisha mifumo ya mwili kufanya kazi vizuri

Unaweza ukajiuliza ni vyakula gani hivyo ambavyo vinafanya kazi zote hizo mwilini?
Usipate shida, nitakufundisha kila kitu kwenye video hii. Chakufanya kama ndio mara ya kwanza kutazama video za channel hii basi Subscribe na kisha bonyeza alama ya kipengele itakayojitokeza, pia usisahau ku-Like na share ili Tuwafikie Wafugaji wengi. Vilevile unaweza kuuliza chochote kwenye comment na sisi tutakujibu.

Vyakula hivyo ambavyo huchanganywa na kukupa mlo kamili wa kuku wa kienyeji ni kama vifatavyo

Vyakula vya Kulinda mwili dhidi ya magonjwa ni Vitamin ambayo hutokana na Mimea kama Azolla, hydroponics, mchicha, Lucina na mimea yote ya kijani au unaweza kuchanganya ambayo imeandalia maalumu (premix)

Vyakula vya Kuupa mwili nguvu ni Carbohydrates/Wanga ambayo hutokana na nafaka kama mahindi, mtama, ngano, na pumba zote za nafaka

Vyakula vya kujenga mwili ni Protein ambayo hutokana na mashudu ya alizeti, karanga na pamba, Soya, Dagaa (Fishmeal) na damu ya wanyama iliyoandaliwa maalumu kwaajili ya chakula cha kuku

Vyakula vya kuupa mwili joto ni Fats/ Mafuta vyakula Vyenye mafuta kama Alize, karanga, pamba, nazi na mashudu ya vyote nilivyotaja

Vyakula vya Kuimarisha mifupa ni Madini mbalimbali ambayo hutokana na Unga wa mifupa ya wanyama na samaki na Chokaa kama Calcium, Iron, Phosphorus, Zinc n.k

Na Maji safi na salama, ambayo
Husafisha na kurahisisha mifumo ya mwili kufanya kazi vizuri

Vyakula vyote nilivyo taja vikichanganywa kwa utaratibu maalumu na kutengeneza Digestible Crude Protein (DCP) ya 18% - 20% chakula hicho kinaitwa stater/Chick Mash ambacho wanapewa vifaranga walio na umri wa siku 1 mpaka wiki 8 na wanatakiwa kulishwa kwa utaratibu maalumu .

Utaratibu wa kuwalisha vifaranga wa kienyeji ni kama ufatao.

Wiki ya 1 na 2 walishe chick stater bila kuwapimia, wape wale tuu kadri watakavyo chakula kikiisha kwenye feeder waongezee. Kufanya hivyo kutawasaidia kuimarisha kinga ya mwili ili kuwaepusha na magonjwa nyemelezi, kujenga mwili na vifaranga watakuwa kwa haraka.
Ukiweza kumudu gharama kwa kipindi hiki cha siku 14, walishe stater ya pillet vifaranga watakula chakula chote bila kubakisha na wataimarika kwa haraka sana.

Wiki ya 3 mpaka wiki ya 7, endelea kuwalisha Vifaranga stater lakini ukiwa unapima kiasi cha kuwapa kwa siku husika.
Wiki ya 3 wape gramu 25
Wiki ya 4 wape gramu 31
Wiki ya 5 wape gramu 36
Wiki ya 6 wape gramu 41
Wiki ya 7 wape gramu 45
Wiki ya 8 wape gramu 49
Wiki hii ya 8 ni wiki ambayo unatakiwa kuanza kuwazowesha chakula cha grower mash kwa kuchanganya kiasi kidogo kidogo kwenye stater ya siku husika.
Mfano kama vifaranga wanakula kilo 5 kwa siku, changanya stater kg 4 na grower kg1. Endelea kuongeza grower na punguza stater mpaka itakapokuwa imeanza wiki ya 9, chakula chako kiwe ni grower mash pekee.

Ukiwalisha Vifaranga wako kwa utaratibu huu utaona matokeo ya ukuaji wao na jinsi ambavyo hawatakuwa wakishambuliwa na magonjwa.

Nikualike kwenye darasa la ufugaji wa kuku aina zote litakalo anza tarehe 10 mwezi wa 8, darasa linafanyika Mtandaoni kupitia group la what's app. Kujiunga na darasa hilo tuma 5,000 kwenye namba unayoiona kwenye screen 0656528455, kisha tuma meseji ya jina na namba yako ya what's app.

Видео JINSI YA KUWALISHA VIFARANGA WA KUKU WA KIENYEJI WAKUWE HARAKA канала Changamkia Fursa
Показать
Комментарии отсутствуют
Введите заголовок:

Введите адрес ссылки:

Введите адрес видео с YouTube:

Зарегистрируйтесь или войдите с
Информация о видео
1 августа 2020 г. 10:00:33
00:07:36
Яндекс.Метрика