Загрузка...

Bondia Terence Crawford atua Arusha, ataja anachotamani, TTB yatoa neno

TERENCE CRAWFORD: ".....natamani kuwaona Simba"

Bondia Terence Crawford kutoka Marekani muda huu yuko Arusha akiendelea na ziara yake yenye lengo la kutangaza utalii wa Tanzania.

Terence amesema amekoshwa na kila kitu alichokutana nacho Tanzania hadi sasa, huku akiwataja wanyama ambao anatamani kuwaona katika ziara hiyo.

Naye mwakilishi kutoka Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Paulin Mkama, ameeleza kuhusu ratiba kamili ya bondia huyo, maeneo yote atakayokwenda, na aina ya chakula atakachokula.

Mingoni mwa sifa za bondia huyo ni kwamba alikuwa bingwa wa dunia kwenye madaraja matano tofauti ya uzito.

Lakini pia aliwahi kumiliki mikanda mikubwa minne kwa wakati mmoja (undisputed champion) kwenye madaraja matatu ya uzito tofauti.

Mwaka jana, bondiaTerence Crawford alimpiga Canelo na kufikisha rekodi ya mapambano 42 ya ushindi bila kupoteza.

Kujua zaidi kuhusu ziara ya bondia huyu, usicheze mbali na Azam TV.

#Vitasa #Ndondi #TerenceCrawford #Ngumi

Видео Bondia Terence Crawford atua Arusha, ataja anachotamani, TTB yatoa neno канала Azam TV
Яндекс.Метрика
Все заметки Новая заметка Страницу в заметки
Страницу в закладки Мои закладки
На информационно-развлекательном портале SALDA.WS применяются cookie-файлы. Нажимая кнопку Принять, вы подтверждаете свое согласие на их использование.
О CookiesНапомнить позжеПринять