Загрузка...

MWILI WA KICHANGA WAOKOTWA DAMPO MBOZI

#HABARI: Wakazi wa Mtaa wa Msaki uliopo Kata ya Ichenjezya wilayani Mbozi mkoani Songwe wamekumbwa na hali ya taharuki baada ya mwili wa mtoto mchanga mwenye jinsia ya kike anayekadiriwa kuwa na umri chini ya miezi tisa kukutwa ukiwa ndani ya bahasha kubwa na kutupwa kwenye dampo la takataka lililopo kwenye mtaa huo.

Mashuhuda wa tukio hilo wakiwemo wafanyakazi wanaozoa taka katika dampo hilo na kuzipeleka dampo kuu wamesema mwili wa kichanga hicho umegundulika majira ya asubuhi ukiwa umefunikwa na bahasha kubwa huku ukiwa umeanza kuharibika kutokana na kunyeshewa na mvua baada ya kutupwa.

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Masaki lilipo dampo hilo Bi Sifa Nassor amesema hilo ni tukio la pili kutokea katika dampo hilo huku akiomba Mamlaka kufanya utaratibu wa kulihamisha kwani lipo jirani na makazi na uzoaji wa taka umekuwa ukichelewa na kuhatarisha afya zao.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Augustino Senga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa uchunguzi mkali unaendela ili kubaini na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria aliyefanya kitendo hicho ambacho amesema hakikubaliki kwa jamii.

Видео MWILI WA KICHANGA WAOKOTWA DAMPO MBOZI канала ITV Tanzania
Яндекс.Метрика
Все заметки Новая заметка Страницу в заметки
Страницу в закладки Мои закладки
На информационно-развлекательном портале SALDA.WS применяются cookie-файлы. Нажимая кнопку Принять, вы подтверждаете свое согласие на их использование.
О CookiesНапомнить позжеПринять